.post-body{ -webkit-touch-callout: none; -khtml-user-select: none; -moz-user-select: -moz-none; -ms-user-select: none; user-select: none; }

0

Kuna malalamiko ya foleni kwenye miji mikubwa Duniani, hii ishu hata Dar ipo pia.. ukacha hilo kuna ishu ya parking.. inawezekana umejenga au unaishi kwenye nyumba yako ya kawaida kabisa lakini una changamoto wa wapi pa kupaki gati yako !!
Teknolojia haiko mbali na sisi kila siku, ubunifu unaofanywa hautaacha wakati mwingine kutushangaza pia.. timu ya Engineers Ujerumani wamefanya ufundi wao, wamekuja na hii gari ndogo ndogo yani.. na bado ina uwezo wa kubonyea ikawa ndogo zaidi.
Hii gari ni ya umeme, ina uwezo wa kusafiri mpaka kilometer 70 kwa battery yake ikiwa full charge kabisa !! Kingine ni kwamba ina uwezo na kupungua upana wake kwa kama centimeter 80 hivi, tyre zake pia zinageuka upande wowote unaotaka sio kama gari nyingine.. kama sehemu ya parking ni ndogo haitoshi basi hii inajipenyeza na inatosha kabisa.
Wapo waliovutiwa na ubunifu huu, Kampuni ya Mercedes Benz wao wamethibitisha kuipenda hii, ndani ya miaka 4 ijayo watakuwa na gari ambalo litakuwa na muundo kama huu.. General Motors pia wamesema mpaka 2020.
Video yake unaweza kuiona hapa.(https://www.youtube.com/watch?v=69Om1_I09ow#t=14)
                       

Post a Comment

 
Top