Mabadiliko
ya teknolojia ya mawasiliano yanayotokea duniani yamekuwa yakileta athali
chanya na hasi ndani ya jamii hasa katika maswala ya mawasiliano.
Wavumbuzi
na wataalamu wa program tumishi duniani nao hawako nyuma katika kubuni programu
ambazo zitawafanya wachumba ama wanandoa wanaotumia simu za kisasa na tabiti
kuwa karibu zaidi katika masuala ya mawasiliano.
Kwa
sasa kuna program tumishi nyingi ambazo ni maalum wa wapenzi ama wanandoa japo
kuwa kuna zile ambazo zinaleta tija zaidi ya nyinginezo.
Couple
Kanuni
iliyoko katika program tumishi ya Couple ni kwamba inawawezesha watu wawili
kuwa na wigo wa mawasilino ya mahusiano yenye faragha kwa kubadilishana picha,video,ama ujumbe wa sauti
Hii
ni program tumishi ina huduma ya kutuma ujumbe wa papo kwa papo kama ilivyo
katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp,picha inaweza kutumwa ikiwa imewekwa
katika mpangilio wa kutoweka baada ya muda fulani pia ina huduma ya kukupatia
taarifa ya mahali pa faragha
ambapo mnaweza kwenda kwa ajili ya chakula ama maongezi ya wachumba ama
wanandoa,ikiambatanisha na kalenda.
Mpaka
sasa inatumiwa na wanandoa zaidi ya milioni mbili duniani ni moja ya program
tumishi ambayo inaonekana kuwafaa wanandoa katika mawasiliano binafsi ya
faragha.
Couple Tracker
Imekuwa ni jambo la kuumiza kwa baadhi ya watu walioko kwenye mahusiano.Jambo hili limekuwa likileta lawama na kushutumiana katika suala kukosa uaminifu.
Couple
Tracker ni program tumishi iliyokusudia kutatua tatizo la watu kutokuwa
waaminifu kwenye mahusiano na
imekusudia kuwa na mkakati wa kusaidia kuboresha uaminishi kwenye mahusiano ya
wachumba ama wenzi wa maisha.
Kinachofanywa
na program hii tumishi ni kumwezesha mwanandoa kuona simu
zilizopigwa,kupokelewa,ujumbe mfupi wa maneno,anachofanya mwanandoa mwenzake
kwenye mitandao ya kijamii ya
Whatsapp, Facebook na uwezo
kutambua mahali simu ya mwanandoa ama mchumba mwenzako ilipo,japo kuwa ina
sehemu fulani ya faragha hata hivyo mawasiliano yote ya masaa 24 katika siku
saba yanaweza kuoneshwa kwa kupitia program hii.
Hata hivyo ni
lazima uhakikishe kuwa kuna makubaliano rasmi ya wahusika wawili kuitumia kwa sababu ya sheria
zinazozuia udukuzi wa mawasiliano.
Our Groceries
Watalaamu
wa mahusiano wanaeleza kuwa maisha ya ndoa baada ya fungate huwa yanachangamoto
zake hasa katika masuala ya kipato katika matumizi mbalimbali ya fedha za
kujikimu kwa wanandoa.
Kila
mmoja analojukumu la kuhakikisha masuala ya manunuzi ama gharama za matumizi ya
nyumbani mfano malipo ya umeme,maji ,malipo na manunuzi ya vifaa mbalimbali vya
familia.
Our
Groceries ni program tumishi ambayo inajaribu kutoa suruhisho la kutatua
upangaji wa bajeti kwa wanandoa na hivyo kuepusha manunuzi ambayo unaweza
yafanya wakati ambapo mwenzi wako ameshayafanya kwa kuwa inakupa taarifa ya
kile mwenzako alicho kinunua kabla.
Kwa
kutumia progam hii unaweza kutayarisha orodha ya mahitaji unayopanga kununua
ama kuyafanyia malipo na ukamshirikisha mwenzi wako kuona orodha hiyo na utakapofanya malipo ama kununua
chochote basi itatuma taarifa kwa kifaa cha mawasiliano cha mwenzi wako na kama
unahitaji kutoa taarifa anunue
bidhaa yoyote unaweza fanya hivyo pia.
Avocado
Kama ilivyo
program tumishi ya Couple, Avocado inawezesha kuwapatia wanandoa mawasiliano ya
faragha na kuwaunganisha katika mawasiliano muda wote.
Unaweza
kumtumia mwenzi wako ujumbe mfupi wa maneno,video,sauti na imewekewa kalenda
ambayo hukumubusha matukio muhimu ya kuyakumbuka ikiwemo siku ya kuzaliwa,siku
ya kufunga ndoa na mambo mengine muhimu kwa wanandoa.
Kwa wale
waliona mahusiano yanayotenganishwa na umbali inasaidia kukufanya uhisi kuwa
karibu na umpendaye,pia inawezesha kutoa taarifa kwa mwenzi kuwa karibu betri
ya kifaa cha mawasiliano itazima,programu hii pia inamwezesha mtumiaji kuona
ujumbe,picha na taarifa zingine hata kama haujaunganishwa na upande mwingine wa
mwenzi wako.
Inawezesha
pia kuficha taarifa za mtumiaji ili mtu mwingine asizione ama kuzipata.
Post a Comment