Kama
ulikuwa unafikiri kwamba itachukua muda kwa HTML5 kutumika zaidi kwenye
mobile app basi unajidanganya. Ukweli ni kwamba HTML5 imekubalika na
wataalam wengi wa IT duniani kote kama standard kutenegeneza mobile
apps. Hii ni kwasababu HTML5 tayari ni web-based standard, tofauti na
language nyingine. Application programs nyingi zina uwezo wa kufanya
kazi vizuri kwa kutumia browser ambayo imeandikwa kwa kutumia HTML5.
Faida
kubwa ya kutumia HTML5 ni developer anaweza kutengeneza HTML5 app
inayoweza kufanya kazi kwenye simu yoyote ya mkononi yenye browser
nzuri. Hii itaondoa lile tatizo lililopo kwamba app iliyotengenezwa kwa
ajili ya platform za simu kwa mfano Android haiwezi kufanya kazi kwenye
platform nyingine kwa mfano iOS. Kwa kutumia HTML5 hili tatizo litakuwa
halipo tena.
Hadi
sasa Linkedln na Pandora zimeshaipitisha HTML5 kama standard ya
kutengeneza applications zake. Miaka kadhaa iliyopita Steve Jobs wa
Apple alitabiri kwamba HTML5 kuwa standard ya web apps. Apple waliamua
kuipa kisogo Adobe Flash kutoka
kwenye platform ya iOS. Kwa sababu Adobe Flash ni plug in application,
kumekuwa na shida kwa wengi kutumia application kama You Tube ambayo
inatumia Adobe Flash. HTML5 imeondoa tatizo hili, huhitaji tena Adobe
Flash kwa sababu una uwezo wa kutumia video moj kwa moja.
Tatizo
linaloikwamisha HTML5 kwa sasa ni jinsi program hii itaweza kuuungana
vizuri na simu za mkononi zilivyotengenezwa ili kuhakikisha inatumia
features zote zilizopo. Hiiinahusiana na features kama kamera, global
positioning system (GPS), n.k. Ikumbukwe kwamba application za kawaida
za simu zinahusiana vizuri na software ya simu kama vile Android. Hii
iniwezesha application hiyo kujenga uhusiano na hardware yenyewe
inayoiwezesha kutoa huduma mbali mbali kwa mfano kujua mteja alipo,
kutoa direction kwa kutumia ramani, n.k
Kuna mengi mazuri ya HTML5 yanakuja hivyo usiisahau kwenye vitu unavyotakiwa kuvijua japo kidogoKutoka blog ya teknolojia :
Post a Comment