.post-body{ -webkit-touch-callout: none; -khtml-user-select: none; -moz-user-select: -moz-none; -ms-user-select: none; user-select: none; }

0

RAPPA Kanye West wa nchini Marekani jana ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima kutoka Taasisi ya Sanaa ya Chicago nchini Marekani.

Kanye akitoa hotuba yake katika taasisi hiyo.
Kanye West aliyeacha chuo akiwa na umri wa miaka 20 na kuamua kuingia kwenye muziki kisha kutoa albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la 'The College Dropout' kwa sasa atakuwa akiitwa Dk. West.
Kanye hakuweza kuficha furaha yake kwa kuachia tabasamu wakati akielekea kutoa hotuba katika taasisi hiyo ambayo ni mojawapo ya taasisi zenye heshima kubwa katika sanaa nchini humo.

Ujumbe alioutuma Kim kwa mumewe Dk. West.
Wakati wa tukio hilo, mke wa staa huyo, Kim Kardashian alikuwa nchini Brazil lakini hakusita kuungana na mumewe kupitia mitandao ya kijamii akimtakia heri kwa kuandika: "Dk. Kanye West!!!! ninajisikia fahari kutokana na wewe mpenzi na nina imani mama yako naye angejisikia fahari pia"

Mama mzazi wa Kanye, Dk. Donda West ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa Profesa wa Kiingereza wa Chuo Kikuu cha Clark Atlanta na baadaye alikuwa Mwenyekiti wa Idara ya Kiingereza Katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Chicago.

Post a Comment

 
Top