Ukuaji
wa Sekta ya TEHAMA umekuwa wa mafanikio na msaada mkubwa katika kuharakisha,
kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuchangia kikamilifu katika kukuza uchumi na kuleta
maendeleo ya Taifa letu. Kwa mfano, wananchi walio wengi sasa wanapata huduma
mbalimbali za mtandao kwa kutuma na kupokea pesa; kulipia ankara za maji, umeme
na tozo mbalimbali kama vile ada na leseni; na mawasiliano ya simu na intaneti
pamoja na elimu mtandao na tiba mtandao.
Palipo
na mafanikio hapakosi changamoto. Pamoja na kwamba tumeshuhudia manufaa na
umuhimu wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika nyanja
mbalimbali ikiwemo ya elimu, afya, biashara, miundombinu ya mawasiliano, pia
kumekuwepo na changamoto ya matumizi mabaya ya mtandao katika ngazi ya mtu
mmoja mmoja, baina ya makundi ya watu na hata kutoka Taifa moja kwenda Taifa
lingine kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni.
Baadhi
ya mifano ni pamoja na suala la wizi wa
fedha kwa njia ya mtandao, matukio ya uhalifu kwa kutumia mtandao, uvujaji wa
taarifa za siri, upotevu wa haki miliki na matumizi ya saini na ushahidi,
mmomonyoko wa maadili, athari za makundi maalumu kama vile watoto na usalama wa
miundombinu mbalimbali ya TEHAMA ambapo Serikali imeingia gharama kubwa
kuiweka.
Wakati
hayo yakijiri, Kwa sasa kumekua na wimbi kubwa la kurubuni watu kupitia
mitandao ambapo majina ya wanasiasa, wanamuziki na wenye majina makubwa
yameendelea kutumiaka vibaya katika mitandao ili kufanikisha urubuni wa kuwaibia
watu pesa kwa kutumia jina la “VIKOBA” – Chakushangaza zaidi kurasa hizo zinazo
onekana zaidi kupitia mitandao yakijamii zinaonekana zimedhaminiwa ili kuweza
kusomwa na wengi kitu ambacho
kinapelekea kuonyesha jinsi gani wimbi hili na wahalifu hawa mtandao
wamejipanga.
Watanzania
hawanabudi kuwa makini sana na kuwa waangalifu sana wanapo takiwa kuingiza
taarifa zao binafsi na wanapo takiwa kufata maelekezo wa kutekeleza miamala
kupitia mitandao kwenye vyanzo vyenye utata.
Kumekua
na malalamiko mengi kuhusiana na wimbi kubwa la watanzania waki lalamikia
kuibiwa/ Kutapeliwa pesa zao kupitia mitandao ya kijamii (kwa njia ya Vikoba)
liwe ni somo kwa wengine kuwa makini zaidi kwenye hili.
Aidha,
Jingine linalo kuja kwa kasi ni usambazaji wa picha na maneno yasiyo rafiki
kwenye mitandao ya kijamii bila na kua na uoga ya kuwa kwa kufanya hivyo
inaweza kusababisha uvunjifu wa Amani katika taifa. Kwenye hili tumeshuhudia
picha mbali mbali na hata maneno ya chuki, ifitinishaji na uchochezi ambayo
yanatishia sana hali ya utulivu iliyopo nchini.
Bado
kumeendelea kuonekana uhalifu mitandao nchini ukichukua sura tofauti mara kwa
mara huku wahalifu mtandao ambao idadi ya wahalifu hao kuonekana kua ni wazawa inaongezeka
kila kukicha.
Kwa
mazingatio hayo ni vizuri watanzania wakatambua kua Wizara ya Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, imechukua jukumu na
kuandaa muswada wa Sheria za Matumizi Salama ya Mtandao kwa lugha ya kiingereza
zinafahamika kuwa ni Cyber Laws.
Muswada
wa Sheria hizo ni pamoja na muswada wa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi (The
Personal Data Protection Bill); na muswada wa Sheria ya Biashara Miamala ya
Ki-elektroniki (Electronic Transaction Bill) na muswada wa Sheria ya Kuzuia
Uhalifu kwa Njia ya Kompyuta na Mtandao (Computer and Cyber Crimes Bills).
Sheria hizi zitajikita katika masuala ya kudhibiti uhalifu kwa kutumia
mitandao, udukuzi, utunzaji wa taarifa, kuwalinda watoto dhidi ya matumizi
yasiyofaa ya intaneti na malipo kwa njia ya mtandao.
WITO: Sheria
mtandao zinatofautiana sana na sharia nyingine kutokana na kukua na kubadilika
kwa teknolojia ya habari na mawasiliano mabapo mabadiliko na ukuaji wake ni wa
kasi sambamba kabisa na ukuaji na ubunifu wa njia mpya za uhalifu mtandao.
Kwakuzingatia hili Sheria hizi zimekua zikipitiwa na kurekebishwa mara kwa mara
ili kuendana na mabadiliko husika. Ni vyema hili likatambulika ili kuhakiki sharia
husika zinaingizwa katika vitendo mapema kabla ya kufikia muda wa kuzipitia
il-hali bado hazijaanza kutumika.
Aidha,
Kama ilivyo kwa matukio mengine yote ya uhalifu na uvunjifu wa amani katika
nyanja nyingine wakati tukiendelea na uandaaji wa sheria, wananchi wanashauriwa
kutoa taarifa kwa vyombo vya udhibiti kuhusu matukio yoyote ya ukiukwaji na
matumizi mabaya ya mtandao na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ili hatua
stahiki ziweze kuchukuliwa kulingana na sheria na kanuni zilizopo sasa.
Mwisho, napenda kuungana na wengine kwa kutoa rai kwa wananchi wote kuwa wajiepushe na matumizi mabaya ya mitandao na badala yake watumie vizuri mitandao hiyo kwa manufaa yao wenyewe, ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Post a Comment