Katika mazingira ya sasa ambapokaribu kila kitu na kila sekta mambo
yanaendeshwa kwa teknolojia ya
mawasiliano kwenye simu, kompyuta,
tabiti, saa, miwani, nguo na hasa
tunapotazamia kila kitu hivi karibuni,
haishangazi kwamba mara kwa mara
watu wanajitokeza kuonesha hofu juu ya
athari za kiafya za vifaa hivi na hata
kuzihusisha na kansa (Saratani).
Kwa muhtasari tu, wanasayansi na
wataalamu wa afya duniani wanakubaliana
kwamba hakuna utafiti uliofanikiwa
kubainisha wazi jinsi simu na vifaa vingine
vya kielektroniki vinavyotoa mionzi
vinavyohusiana na saratani kama ambavyo
watu wa kawaida wamekuwa wakihofia.
Mionzi
Teknolojia yetu ya mawasiliano ya sasa
inahusiana sana na mionzi – vitu
visivyoonekana kwa jicho la binadamu na
hata kuhisiwa. Vifaa vyetu hivi vyote, simu,
tabiti, saa-janja, hedifoni zisizo na waya,
luninga, redio za FM na AM vyote hutoa
mionzi ya ‘bluetooth’, wayalesi, LTE na
microwave, waya za umeme na hata DUNIA
na JUA lenyewe linatoa mionzi!
Suala la muhimu kutambua ni kwamba,
mionzi yote haiko sawa na kuna baadhi ya
njia za kuzitofautisha na ya muhimu zaidi
kwenye mada hii, husika na kichwa cha
habari hapa juu ni ‘ionization’ – yani uwezo
wa mionzi kutoa elektroni kwenye atomu –
ambayo ni chembe chembe inazotengeneza
chochote chenye uhai na kisichokuwa na
uhai.
Kuna ‘ionizating radiation’, yani mionzi
inayoweza kutoa elektroni kutoka kwenye
atomu na ‘non-ionizing radiation’, yani
mionzi isiyoweza kufanya hivyo.
Celli za Mwili
Kwenye sayansi, kama atomu moja ikipoteza
elekroni, haina shida kwani itaweza
kushirikiana na atomu nyingine kuipata
‘balance’ yake ya elektroni. Binadamu, kwa
upande mwingine, anatengenezwa na atomu
nyingi zilizofungamana (molecule) na zenye
ushirikiano wa kikemikali zaidi ya atomu
zilizo kivyakevyake. Elektroni zikitenganishwa
kutoka kwenye moleculi, vitu mwilini huacha
kufanya kazi kama vinvyotakiwa.
Kuna moleculi moja ambayo ikiharibiwa na
‘ionzing radiation’, shida kubwa itazuka
mwilini. Moleculi hiyo ni muhimu katika
kutoa muongozo wa jinsi celli zinavyofanya
kazi na inaitwa DNA (deoxyribonucleic acid).
Wakati Celli inajigawa – kitu ambacho
kinatokea kwa kawaida karibu mara trillioni
mbili kwa siku ndani ya mwili wa binadamu,
DNA inajigawa sawia kwa kila celli
itakayotokea hapo. Na wakati yai linapo-
ungana na celli ya mwanaume, nusu ya kodi
kutoka kila celli hungana kutengeneza kodi
mpya – binadamu mpya.
DNA na Mionzi
Kuna uwezekano saa nyingine, kwamba
mambo yakaenda kinyume na yanavyotakiwa
kwenye kugawanyika kwa celli na hapo ndipo
kunaweza kutokea celli isiyo na uhai (dead
cells) ambayo inajiunga pamoja na celli
zingine mfu kutengeneza ngozi na hatimaye
kutoka nje ya mwili au katika maana ya
uzazi, kizazi kisicho na uhai. Kuna mara
chache sana, katika mchakato huo huo,
zinatokea celli ambazo siyo mfu ila hazifanyi
kazi vizuri. Hapa ndipo anapozaliwa mtu
mwenye upungufu au inapoanza kansa
(saratani).
Hatahivyo, mara nyingine ikitokea hali kama
hii, tunapata mabadiliko chanya ya celli
ambayo yanaweza kubadili mwenendo wa
jamii ya viumbe husika.
Mionzi yenye uwezo wa ku-’ionize’ inaweza
kutoa elektroni kwenye moleculi za DNA. Kitu
hiki kikitokea, kinaweza kupelekea celli kufa
au kupelekea DNA kukosa uwezo wa kutoa
muongozo kwa celli hiyo na hivyo celli
huendelea kuishi ila vivyo-sivyo na
kupelekea kansa. Na kama uharibifu
ukifanyika kwa namna flani inayoruhusu, basi
celli hiyo itaweza kujiongeza na hatimaye
uvimbe(tumor) utatokea kwenye sehemu ya
mwili na hatari zaidi itatokea iwapo celli hiyo
ikisambaa sehemu nyingine mwilini.
Mionzi na Vifaa vya Kielektroniki:
Redio ya simu yako inatoa mionzi ya nguvu
kati ya masafa ya MHz700 – GHz2.5.
Wayalesi inafanya kazi kati ya GHz 2.4 – 5.
Bluetooth nayo inacheza kwenye masafa ya
GHz 2.4 pia. Hata katika nguvu ya juu kabisa
ya vifaa vyetu vya kielektroniki vinafanya kazi
kwa nguvu ya chini ya 1/1200 ya nguvu ya
mwanga na 1/9600 ya nguvu inayohitaji
ku-’ionize’ au kuchana elektroni kutoka
kwenye atomu ambayo ni terahertz 2400. X-
ray inatoa nguvu mara millioni 12 ya nguvu
inayotoa simu yako na pia mionzi ya gamma
ambayo ina madhara.
Tafiti mbalimbali , Wanasayansi na hata
Madaktari Wanakubali kuwa Hakuna
Shida:
Kwa mfano, Taasisi ya Saratani ya Marekani
(National Cancer Institute at the U.S. National
Institutes of Health) inakubaliana ya kwamba
“there is no evdence from studies of cells,
animals, or humans that radio frequency
energy can cause cancer.” Kwa kiswahili,
wanasema hakuna ushahidi kutoka tafiti za
celli, wanyama au binadamu zinazoonesha
masafa ya redio yanaweza kuzua saratani.
The American Cancer Society nao wansema,
“the RF waves given off by cell phones don’t
have enough energy to damage DNA directly
or to heat body tissues”. Yani, mionzi
inayotolewa na simu haina nguvu ya kutosha
kuharibu DNA moja-kwa-moja au kuunguza
kiungo vya mwili. Tafiti ya miaka 20 ya
Jarida la Epidemiology *(The Journal of
Epidemiology) ya nchi za Scandinavia
hazikupata uwiano kati ya matumizi ya simu
na saratani. Tafiti ya nchini Denmark ya
Swiss Tropical and Public Health Institute
ililinganisha uwezekano wa kupata saratani
kati ya watumiaji wa simu na wasio watumiaji
kutoka mwaka 1990 hadi 2011 na kukuta
kwamba hakuna muongezeko wa hatari ya
kupata saratani.
Cha Msingi:
Kiukweli, kibaya kinachoweza kufanywa na
simu yako ni kuongeza kidogo joto la mwili
na hata hivyo, hilo joto lote linatoka kwenye
vifaa vya kieltroniki na betrii, na sio mionzi.
Kama kawaida, kila kitu kizuri hakiwezi
kukosa ubaya. Simu zetu na vifaa-kompyuta
vya kisasa vinatuwezesha kushirikiana kwa
karibu zaidi na kukamilisha shughuli zetu za
kila siku kwa ufanisi zaidi ila, ubaya wake
unaonekana hasa kijamii na kitamaduni.
Inaweza kukubalika kwamba vifaa hivi
vinapunguza jinsi tunavyoshirikiana na watu
karibu yetu. Si rahisi kuboreka na kukosa
kitu cha kufanya unapokuwa na simu ya
mkononi ya kisasa. Haulazimiki kuongea na
mtu unapokuwa unasubiria gari kituoni au
hata huduma hospitalini. Mazungumzo kati
ya binadamu yanapungua na hata uwezo wa
kuanza na kuendesha mazungumzo
unapungua siku hizi. Pia, pamoja na mambo
mengine kama uwezo wa kuandika lugha
fasaha, uvumilivu, simu na teknolojia ya
mawasilano inabadili tamaduni zetu kutokana
na urahisi wa mawazo ya kigeni kuingia
kwenye jamii yetu ya kisasa ila katika suala
la saratani, simu haziwezi kuhusishwa.
Post a Comment