.post-body{ -webkit-touch-callout: none; -khtml-user-select: none; -moz-user-select: -moz-none; -ms-user-select: none; user-select: none; }

0

SOMA KWA MAKINI SANA …. chukua tahadhari na wala usipuuze kwani utaumia

Je ni mmoja kati ya watu ambao wame-save namba za akaunti zao za benki na maneno siri kwenye simu yako? Na sio tu akaunti za benki au maneno siri bali taarifa zako zingine za siri umeziweka kwenye simu yako?  Ikiwa hivyo, basi unashauriwa kuzifuta haraka sana. Unauliza kwanini? Basi sikia sasa.
Dunia ya sasa ambayo ni ya teknolojia mtu anaweza fanya chochote akiwa mbali ili mradi tu apate namba ya simu yako. Ndio, nambari yako ya simu tu, inaweza kumfanya mtu akusanye taarifa zako zote katika simu yako.
Hivi ulishawahi kupigiwa simu kwa moja ya nambari zifuatazo?  +375602605281 au 37127913091 au +919911458416 au namba yoyote inayoanza na +375 au +371? Je ushawahi pigiwa? Je ushabipiwa? Ikiwa hujawahi kupigiwa, basi ukipigiwa tafadhali usipokee, na ikiwa hujabipiwa, basi ikitokea siku umebipiwa, usithubutu kutaka kumpigia mhusika.
Hizo ni baadhi tu kwani zipo namba nyingi za namna hiyo. Unapopigiwa simu hii mpigaji huwa haongei, we utapokea na kusema "hallow" …. yeye hataongea lolote na atakata simu hiyo. Unajua nini kinafuatia baada ya hapo?
TeamViewer_logKitendo cha sekunde tatu au nne yeye kule tayari anakua na uwezo wa kunakili nambari zako zote za simu zilizo katika orodha yako ya nambari za simu kwenye simu yako. Anaweza pia kunakili ujumbe mfupi wa maneno uliohifadhiwa katika simu hiyo, na kama ziko taarifa za benki, maneno siri na taarifa zingine zote muhimu, anaweza kuzinakili kwa muda huo tu. na baada ya hapo, ikiwa atahitaji kuchukua hata fedha kwenye akaunti yako ni rahisi, tena bila ya yeye kwenda benki wala wewe kujua.
Unaweza ukalipuuzia hili au ukalifanyia kazi, yote ni sawa, ila yakikutokea, usijesema hukujulishwa mapema. Technology imekua sana siku hizi, na wezi wamekua wabunifu sana pia. 
Hivi kwa mfano unaamini kuwa hata mimi binafsi nina uwezo wa kujua "menu" ya simu yako yooote kuanzia majina uliyo-save, msg zako, picha, na vingine vyote ikiwa tu nitakuambia ufungue bluetooth na simu yako ubaki nayo hapo hapo lakini mimi kwa kutumia "software" inayoitwa "magic blue hack software" ninakuwa na uwezo wa ku-hack taarifa zako zako kupitia bluetooth yangu nitakayofungua na ku-copy Menu yako yote? Bonyeza hapa kusoma zaidi kuhusu software hii kwa undani. Na zipo nyingi sana zenye uwezo wa ku-hack taarifa za mtu kiundani kuliko hii.
Na kwa taarifa yako tu ni kwamba, hata computer ya tu naweza ifungua na kuitumia kama yangu hata akiwa mbali kama tu nitajua computer yake inatumia "team viewer" yenye namba gani. Kama hujui kuhusu "team viewer" inavyofanya kazi, bonyeza hapa
Leo hii licha ya jitihada kubwa ambazo zimekuwa zikifanywa katika kuimarisha usalama wa taarifa za kimtandao na makampuni mbalimbali yenye kujishughulisha na masuala ya usalama mtandaoni, bado akaunti ya barua pepe ya mtu inaweza kufunguliwa na mtu mwingine japokuwa ni wewe mwenye neno siri la kuingilia kwenye akaunti hiyo.
Sasa ikiwa Mtanzania aliyesoma kidogo tu anaweza kufanya mambo haya, je vipi hao wazungu wenyewe wenye hizi teknolojia? 
Kiukweli Usalama wa mali zako utatokana na umakini wako mwenyewe, hii ni dunia ya wajanja iliyojaa watoto wa mjini. Ukitumia simu ya NOKIA unaweza futa taarifa za simu zilizoingia, zilizotoka, na hata ambazo zilipigwa lakini hukuzipokea. lakini kwa mtu anaejua kucheza na simu akiishika simu yako akaingia sehemu ya "Setting" iliyoandikwa "Sync and Backup" anao uwezo wa ku-restore (kurejesha) kila ulichokifuta.
Mwenye uwezo wa kulinda mali zako ni wewe tu na Si mwingine!

Post a Comment

 
Top