Sean Miles anaingia
kwenye historia, anaingia kwenye headlines pia.. yeye kagundua hii simu
ambayo imetengenezwa kwa majani kabisa pamoja na mchanganyiko wa vitu
vingine vilivyochakaa ama vilivyoharibika.
Dili ambayo alipewa na Kampuni ya O2 ilikuwa Miles afanye
ubunifu njia ambayo wataweza kutumia mabaki ya vitu ambavyo vimechakaa
na havifai kwa matumizi, katoka na hii ambayo hata waliomuagiza hiyo
kazi imewashangaza yani.
Unaambiwa cover ya simu hii ukiiangalia ni kama majani kabisa.
Ubunifu huu umefungua ukurasa mpya kwenye Teknolojia, Kampuni ya O2
wanaangalia kama wataweza kuweka nguvu nyingi zaidi ili simu zenye
cover hizi zilizotengenezewa majani zitengenezwe nyingi na kuingia
kwenye soko la Dunia.
Vipi mtu wangu ukikutana na hii simu pale Kariakoo an Mlimani City kuna kitu kitakufanya usiipende labda?
Post a Comment