Takriban asilimia 40 ya kazi nchini
Australia ambazo zipo kwa sasa huenda zikapotea katika kipindi cha kati
ya miaka 10 hadi 15 ijayo .
Ripoti mpya ya kamati ya maenedeleo ya
kiuchumi CEDA imebaini kwamba matumizi ya mitambo inayojiendesha katika
vizazi vijavyo inaweza kubadilisha nguvukazi ya taifa hilo.Wimbi la mabadiliko ya kiteknolojia halipingiki na linafaa kuchukuliwa kama jeki ya kiuchumi.
Mitambo ya roboti inaweza kuchukua kazi zote kutoka uuguzi hadi upishi,udereva na kuwaosha wagonjwa wazee.
Katika maeneo mengine ya mashambani na majimbo ya Australia zaidi ya asilimia 60 ya kazi zinaweza kupotea kulingana na afisa mkuu wa CEDA Profesa Stephen Martin.
Post a Comment