Kampuni ya chakula Heinz imeomba
msamaha baada ya alama ya siri katika mkebe mmoja wa Tomato Ketch Up
kuwaelekeza wateja katika mtandao wa ngono.
Kampuni hiyo hiyo
imesema kuwa alama hiyo ya siri ilipitwa na wakati na kwamba illikuwa
inatumia kila njia kuhakikisha kuwa kitu kama hicho hakifanyiki tena.Swala hilo liligunduliwa na na Daniel Korell,mteja wake nchini Ujerumani ambaye aliripoti kwa kampuni hiyo.
Swala hilo lilibaini hatari inayoweza kusababishwa na alama hizo za siri kulingana na mtaalam mmoja wa usalama.
Alama hiyo ambayo inaweza kupatikana kwa kutumia simu aina ya Smartphone ili kuweza kuingia mtandaoni ilitakiwa kuwaelekeza wateja katika eneo ambalo watumiaji wanaweza kubuni lebo ya chupa ya Heinz Tomato Ketchup Hot kama mpango wa ukuzaji wa bidhaa hiyo unaofanywa na kampuni hiyo.
Aliripoti kisa hicho akisema kuwa huenda bidhaa hiyo haiwafai watoto wadogo.
Post a Comment