Mawasiano ni jambo muhimu sana kwa maendeleo ya ulimwengu,
njia za mawasiliano ni pamoja na barabara, simu, mazungumzo, ujumbe mfupi,
barua, barua pepe, bahari, reli, tovuti, na vituo vya mawasiliano vingine.
Njia hizo zote za mawasiliano zina faida na ubaya wake.
Hebu na tuangalia VITUO VYA MAWASILIANO, ambavyo wengine
wanasema ndio njia bora zaidi ya kuwasiliana. Kuna mamia ya vituo vya
mawasiliano, na kituo maarufu zaidi-facebook-kinakadiriwa kuwa na washiriki
wapatao milioni 800! “Ikiwa facebook ingekuwa nchi, kwa mujibu wa time
magazine, inasema ingekuwa ni nchi ya tatu kwa ukubwa duniani, baada ya china
na india.” Vituo vya mawasiliano ni nini, na kwanini vimekuwa maarufu sana?
Kituo cha mawasiliano ni tovuti inayowezesha washiriki
kusambaza habari zaokati ya marafiki ambao wamewachagua. Pia kituo cha
mawasiliano hutumika kuwaonesha wenginee picha zako aidha za mahafali, au
safari yako ulivyokwenda likizo kijijini, au matukio mengine.
Kuandika barua kunachukua muda mrefu kufika lakini pia
itakugharimu ikiwa unataka kutoa nakala nyingi ya picha, kupiga simu
kutakugharimu kwa kuwa utalazimika kumpigia mtu mmoja mmojana huenda wengine
wasiwe hewani au wasipokee simu zenyewe na wakawa hawana wakati wa kuzungumza
nawe wakati wewe una muda. Siku hizi si watu wengi wanaojibu barua pepe, na hata wakifanya hivyo huenda
ikachuku majuma mengi hadi mtu kukujibu. Lakini unapotumia vituo vya
mawasiliano, unapachika tu maelezo yako, kuhusu mambo unayoyafanya na marafiki
zako nao watapachika habari na picha zao, na kila mmoja ataweza kuona kwa
haraka taaifa na habari zote pia picha. Na nyinyi nyote mtaweza kupata habari
kwa haraka tena mara moja mnapoingia katika aidha tovuti au kituo hicho cha
mawasiliano na ni rahisi sana hakuna gharama kubwa.
Hilo halimaanishi kuwa mazungumzo kupitia vituo vya
mawasiliano huwa ni upuuzi mtupu. Kwa mfano, msiba unapotokea, kama vile sakata
la mabomu gongo la mboto, mimi nilikuwa katika semina ya walimu iliyoandaliwa
na british council iliyofanyika huko bwawani morogoro, na mafuriko yaliyotokea
juzi mimi nilikuwa jijini Istanbul nchini uturuki, lakini nilizipata kwa haraka
taarifa kupitia vituo vya mawasiliano, na nikaweza kujiona hali halisi kupitia
picha zilipachikwa humo. Watu wengi hutumia vituo vya mawasiliano ili kufahamu
hali za wapendwa wao au kutafuta marafiki wapya nap engine kujua ni kiasin gani
anapendwa.
Ni dhahiri kuwa, kuna faida za kutumia vituo vya mawasiliano,
lakini pia tujiulize, je kuna hatari zozote? Ikiwa zipo, ni hatari gani hizo na
unawezaje kuziepuka?
“Katika wingi wa maneno
hapakosi kuwa na kosa, lakini anayezuia na kuchunga ulimi wake ametenda jambo
la busara zaidi”
VITUO VYA MAWASILIANO
VINAATHIRIJE UNDANI WAKO?
Usipokuwa mwangalifu, habari zako za kibinafsi, picha, ujumbe
mfupi unaopachika kwenye ukurasa wako, na maelezo unayoandika kwenye ukurasa wa
wengine, yanaweza kufunua mambo mengi sana yakuhusuyo ambayo hukuyatarajia. Kwa
mfano, yanaweza kufunua habari kuhusu mahali unapoishi, wakati ambapo upo
nyumbani, ama ikiwa umetoka, mahali unaposoma au kufanyia kazi, habari kuhusu
mahali unapoishi pamoja na ujumbe kama vile “Kesho tunaenda likizo” unatosha
kumwambia adui mahali na wakati wa kukushambulia.
Kufichua habari nyingine kama vile anuani ya barua pepe,
tarehe ya kuzaliwa, au namba yako ya simu kunaweza kufanya udhulumiwe,
uonewe, au kumfanya mtu aibe utambulisho
wako. Ingawa watu wengi hutoa habari hizo kiurahisi katika kurasa zao za vituo
vya mawasiliano.
Watu husahau kwamba mara tu wanapopachikakitu kwenye
intaneti, kinaweza kupatikana na kila mtu. Hata mtu anapofunga ukurasa wake
utumike na watu maalum tuau marafiki pekee, hawezi kudhibiti jinsi marafiki hao
watakavyotumia habari hizo. Kwa kweli chochote ambacho mtu anapachika kwenye
kituo cha mawasiliano afahamu kuwa kinapaswa kuonwa na kuwa ni habari ya umma
au habari ambayo umma unaweza kuipata kwa urahisi zaidi.
VITUO VYA MAWASILIANO
VINAATHIRIJE WAKATI NA FIKIRA ZAKO?
“Mhakikishe mambo
yaliyo ya maana zaidi, maana wakati ni mali”
UNACHOPASWA KUJUA.
Kutumia vituo vya mawasiliano kunaweza kukuibia wakati mwingi sana na
kukukengeusha kutokana na utendaji mwingine muhimu zaidi. Ukiwa na marafiki
wengi ndivyo utakavyotumia wakati mwingi zaidi
katika kituo cha mawasiliano na ni rahisi zaidi kuwa mraibu. Nilifanya utafiti
mfupi kuhusiana na namna watu walivyonaswa na utumiaji wa muda mrefu katika
vituo vya mawasiliano na kusahau kuwa wana majukumu mengine, wasikilize hawa:
“Ni vigumu kuacha kutumia uso wa kitabu-facebook,
hata wakati ambapo hutaki kuendelea kukitumia kituo hicho au umechoka, na
ukiacha ni pale unapokuwa umepitiwa na usingizi” Julieth-Osterbay
“Kuna vitu vingi sana unavyoweza kufanya
humo-michezo, mitihani, kurasa kwa ajili ya watu wanaopenda muziki Fulani, kazi
za ulinganiaji wa kidini, bila kutaja kurasa za marafiki wako, lakini utaacha
yote hayo ya muhimu na kupoteza muda kwa rafiki hata kukiwa hakuna cha
kukijadili” Mwinchumu-Tabata
“Ni uraibu unaokunasa kabisa pasi na mwenyewe
kufahamu, hutambui kuwa umenaswa hadi mama yako anaporudi nyumbani na kukuuliza
kwanini hujaosha vyombo” Hawa-DUCE
“Nilijikuta nikitamani kufika nyumbani upesi kutoka
shuleni na hata saa zingine kuona mwalimu wa kipindi cha mwisho ni kero
darasani ili nikaone ikiwa kuna yeyote ambaye ameandika maelezo yake kwenye
ukurasa wangu au anasubiri kuchati na mimi. Kisha nilihitaji kuwajibu wote hao
na kuangalia picha zote mpya walizopachika. Ilikuwa ni rahisi sana kwangu
kuudhika nilipokuwa nikitumia intaneti, na nilichukia sana mtu aliponikatiza
kwa aidha kunituma au kutaka jambo hata kuniongelesha. Watu Fulani
ninaowafahamu hutumia kituo hichi kila wakati-hata wanapokuwa wamealikwa,
katika vikao, maofisini, madarasani na pia usiku sana, muda wote utawakuta wapo
hewani na ukiwauliza wanakujibu papo kwa hapo!”- Fransis-Mbande secondary
Hakika
utakubaliana name kuwa mara nyingi umekuwa ukifikiria kujisomea, lakini mara
ulipokumbuka kuwa kuna watu watakuwa wamekutafuta fb, ukaachana na habari ya
kujisomea na matokeo yake ukajikita katika kuchati na kupandishwa picha hadi
usingizi ukakupitia
Hakika wakati ni kitu ambacho hupaswi kukipoteza,
KWA HIYO NI JAMBO GANI UNALOWEZA KULIFANYA KUKABILIANA NA HILI?
JAMBO UNALOWEZA KUFANYA.
Wakati ni kitu ambacho hupaswi kupoteza. Kwahiyo,
kwanini usipange jinsi utakavyoutumia, kama unavyoweza kukaa na kupanga namna
utakavyotumia pesa zako baada ya kuzipata? Kwanza, andika kiasi cha wakati
unachohisi kwamba kinafaa kutumiwa kwenye kituo cha mawasiliano. Kisha
jichunguze kwa mwezi mzima na uone ikiwa ulitumia wakati vizuri kama
ulivyopangilia. Fanya mabadiliko yanayohitajika.
Ikiwa wewe ni mzazi na vijana wako wanatumia wakati na muda mwingi kwenye vituo
vya mawasiliano, jaribu kuchunguza ikiwa kuna mambo yoyote yanayochochea tatizo
hilo. Kwa mfano, katika kitabu chake CYBER-SAFE KIDS, CYBER-SAVY TEENA, Bw
Nancy E Willard anasema kwamba kutumia kituo cha mawasiliano kupita kiasi
kunaweza kuhusianishwa na wasiwasi, mfadhaiko, na kutojiheshimu. “Vijana wengi
huwa na wasiwasi kuhusu ikiwa wanapendwa na wengine au la,” anaandika. “Ikiwa
vijana wanapima kama wanapendwa kwa kutegemea wanawasiliana na marafiki wao kwa
kiwango na kadiri gani kupitia vifaa vya kielektroniki, hilo linaweza kuchochea
uraibu.”
Usiache vituo vya mawasiliano-au utendaji wowote wa intaneti-uathiri uhusiano
unaopaswa kuwa ukikuza ndani ya nyumba yako mwenyewe. Jambo moja la kushangaza
kuhusiana na intaneti ni kuwa ingawa inafanya kuwasiliana kuwe rahisi zaidi
wakati ambapo watu wa familia wako mbali, matumizi ya intaneti yanaweza
kuwafanya watu au marafiki watengane wakiwa pamoja kwakuwa kila mmoja
atashughulishwa na marafiki zake wengine wa vituo vya mawasiliano.”
Nafikiri vituo vya mawasiliano ni njia nzuri sana ya kuwasiliana na watu.
Lakini, kama tu kitu kingine chochote, unapaswa kujua wakati wa kuacha
kukitumia.
AFADHALI KUBAKI NI SIFA
NJEMA KULIKO KUW NA MALI NYINGI
Mambo mengi unayoyapachika katika kituo cha mawasiliano
hukufanya uwe na sifa ambazo si rahisi kuzibadili, Ni kana kwamba watu wengi
hawaoni hatari iliyopo. Inaonekana kwamba watu wanapoanza kutumia kituo cha
mawasiliano hupoteza uwezo wao wa kufikiri, wanasema mambo mengi ambayo kwa
kawaida hawangeweza kusema, wanapachika picha zenye mavazi ambayo kikawaida si
muonekano wao. Pengine hawatambui kuwa kupachika kitu kimoja tu kisichofaa kunaweza
kuharibu sifa yako daima.
Post a Comment