.post-body{ -webkit-touch-callout: none; -khtml-user-select: none; -moz-user-select: -moz-none; -ms-user-select: none; user-select: none; }

0

Mambo ya msingi kuhusu intaneti

Wavuti ni nini, na ni jinsi gani unavyoweza kuifanyia kazi?
Unavyochunguza vidokezo juu ya usalama katika Vizuri Kufahamu, unaweza ukawa na maswali kadhaa kuhusu wavuti ni nini na jinsi ya kutumia aina maarufu ya huduma mtandaoni. Tafadhali angalia majibu haya kutoka Googlers na pata maelezo zaidi kuhusu kuingia mtandaoni, kupata maelezo na kuabiri katika mtandao, na kuunganisha na kushiriki mtandaoni.

Kuingia mtandaoni

Intaneti ni nini?

Intaneti ni mtandao wa kompyuta zilizoenea duniani kote zote zikiwa zimeunganishwa moja kwa nyingine. Unapojiunga kwenye Intaneti unakuwa na ufikiaji wa World Wide Web, ambayo ni sawa na maktaba iliyojaa kurasa za maelezo.
Kusoma zaidi, chunguza kijitabu cha Google cha Vitu 20 Nilivyojifunza.

Unaunganishwa vipi kwenye Intaneti? Shughuli ya ISP ni ipi?

Kabla hujaanza kuuchunguza mtandao, utahitaji kuweka mpango na ISP. ISP, au Mtoa Huduma za Intaneti, ni kampuni inayokuruhusu kufikia Intaneti na huduma nyingine za mtandao. Wanatoa njia tofauti za kuunganishwa ikiwa ni pamoja na kupiga simu, kebo, fiber optics au Wi-Fi. Muunganisho hizi tofauti huamua kasi ya ufikiaji wako wa mtandao.

Intaneti inafikaje kwenye simu yangu ya mkononi? Je, ni tofauti kutoka kwa eneo-kazi?

Kwa ujumla, simu ya mkononi huunganishwa kwenye mtandao na mawimbi yasiyotumia waya yaleyale yanayotumika kupiga simu. Simu yako inaunganishwa kwa mnara wa simu za mkononi katika hilo eneo, kisha inakuunganisha kwenye Intaneti. Kwa sababu kuhamisha data kati ya vifaa vya simu za mkononi na Intaneti inaweza ikawa ghali, watoa huduma hutoza kwa mipango ya data.
Vifaa flani, kama vifaa vya simu za mkononi vinavyoendesha Android, vinaweza pia kuunganishwa kwa Mtandao kupitia Wi-Fi. Wi-Fi inakuruhusu uunganishe simu yako, kompyuta ndogo au kompyuta ndogo kwa Mtandao pasipo kutumia waya na bila kuhitaji mawimbi ya simu za mkononi au mpango wa data. Kwa ujumla, muunganisho wa Intaneti katika simu yako ya mkononi una kasi zaidi kupitia mitandao ya Wi-Fi, lakini unapaswa uwe kwenye eneo ambalo Wi-Fi inapatikana. Mikahawa mingi, maeneo ya maduka ya rejareja, na wakati mwingine mijini kote itatoa Wi-Fi bila malipo.

URL, anwani ya IP na DNS ni nini? Na, kwa nini ni muhimu?

URL ni anwani ya wavuti unayochapa kwenye kivinjari ili kufikia tovuti. Kila tovuti ina URL. Kwa mfano, URL hii www.google.com itakupeleka kwenye tovuti ya Google.
Kila URL pia ina anwani ya IP. Anwani ya IP ni mfululizo wa nambari zinazoambia kompyuta yako wapi pa kupata maelezo unayoyatafuta. Anwani ya IP ni sawa na nambari ya simu—nambari ndefu, changamani ya simu. Kwa sababu anwani za IP zilikuwa changamani sana na ngumu kukumbukwa, URLs ziliundwa. Badala ya kuchapa anwani ya IP (45.732.34.353) ili kwenda kwenye tovuti ya Google, unachotakiwa kuchapa ni URL, www.google.com.
Kwa kuwa Intaneti ina tovuti nyingi sana na anwani za IP, kivinjari chako hakijui moja kwa moja ni wapi kila moja wapo ilipo. Inabidi itafute kila moja. Hapo ndipo DNS (Mfumo wa Majina ya Vikoa) inapoingia.
DNS kimsingi ni “kitabu cha simu” cha Mtandao. Badala ya kutafsiri "John Doe" kwenye nambari ya simu, DNS badala yake inatafsiri URL, www.google.com, kwenda kwa anwani ya IP, inakupeleka kwenye tovuti unayoitafuta.

Kivinjari ni nini?

Kama tu unavyoenda katika maktaba ili 'kuvinjari' kupitia vitabu, unaweza kupata au kuchunguza kurasa kwenye Intaneti ukitumia kivinjari cha Intaneti. Kivinjari ni aina ya programu kwenye kompyuta yako inayokuruhusu kufikia Intaneti. Kivinjari huwa kama dirisha linalokuonyesha wavuti mbali mbali ambako maelezo hupatikana. Unachotakiwa tu kufanya ni kuchapa anwani ya wavuti kwenye kivinjari chako na utapelekwa kwenye tovuti hiyo moja kwa moja.

Nawezaje kufanya maandishi kwenye kivinjari changu yawe makubwa (au madogo)?

Wakati mwingine maneno kwenye skrini yako yanaweza yakawa makubwa mno au madogo mno kusomeka kwa urahisi. Ili kubadilisha ukubwa wa maneno kwenye kivinjari chako, bofya na ushikilie kitufe cha [control] au [command] kwenye kibodi yako na ugonge kwenye kitufe cha ongeza [+] au toa[-]. Kuchagua [+] kutafanya maandishi yako kuwa makubwa, na kuchagua [-] kutafanya maandishi yako kuwa madogo.

Navinjari vipi wavuti na vichupo?

Ikiwa unachunguza tovuti moja kwenye kivinjari chako na ungependa kuangalia tovuti nyingine kwa haraka, unachopaswa kufanya ni kufungua kichupo tu. Kimsingi kichupo ni dirisha jingine ndani ya kivinjari kimoja. Kwa kufungua kichupo, unaweza kuruka kati ya tovuti kwa urahisi. Jinsi ya kufungua kichupo itategemea ni kivinjari gani unachotumia. Katika vivinjari vingi, unaweza kufungua kichupo kwa kwenda kwenye [Faili] na kuchagua [Kichupo Kipya].

Nasasisha vipi kivinjari changu?

Matumizi ya toleo jipya kabisa la kivinjari yanamaanisha uvinjari wa kasi na wenye usalama zaidi. Kutambua jinsi ya kusasisha kivinjari chako kutategemea na aina ya kivinjari unachotumia. Kila aina ya kivinjari – kama Chrome, Firefox, Internet Explorer, Safari kutaja tu chache – kitakuwa na mchakato tofauti wa kusasisha. Kivinjari cha Chrome, kwa mfano, kinajisasisha otomatiki kinapotambua kuwa toleo jipya la kivinjari hicho linapatikana. Mchakato wa kusasisha unatokea katika mandhari-nyuma na wala huhitaji kuchukua hatua yoyote kwa upande wako.

Kupata maelezo mtandaoni

Utafutaji unafanya hakika unachosema. Unatafuta. Kwa mfano, ukichapa neno "magari" kwenye injini tafuti ya Google, ombi hilo litatumwa kutoka kwenye kifaa kupitia Intaneti kuja kwetu. Tunaangalia matokeo sahihi ya utafutaji na kuyatuma yarudi kwenye kifaa chako – yote chini ya sekunde moja.
Injini tafuti hutimiza matokeo haya kwa kutambaa na kuorodhesha maelezo yote yanayopatikana mtandaoni. Maarifa ya dunia yanaongezeka mara mbili kila baada ya miaka miwili na changamoto ya kuunganisha watu na kile wanachokitafuta haiwi rahisi – hasa kwa 16% ya utafutaji upya wa kila siku. Wahandisi wanahitaji daima kufanya kazi kwa bidii ili biashara na wateja waendelee kukutana.

Ninapataje maelekezo ya usafiri wa umma?

Ikiwa unahitaji kuabiri basi au kupata njia mkato ya karibu nawe, baadhi ya ramani mtandaoni kama vile Google Maps zinaweza kukusaidia utoke ulipo hadi unapohitaji kuwa. Kwenye Google Maps, chapa anwani ya unakotoka na anwani ya unakoenda. Chagua chaguo la usafiri wa umma – ikoni ya basi – ili kupata maelezo ya usafiri wa umma yanayopatikana.

Ninapataje maelekezo ya kuendesha gari?

Unatafuta kituo cha karibu kabisa cha mafuta katika safari yako ya barabara? Unajaribu kufika nyumbani kwa bibi yako? Kupata maelekezo ya kuendesha, kutembea au kupita ni rahisi. Kwenye Google Maps kwa ajili ya eneo-kazi na kifaa chako cha mkononi, unahitaji tu kuingiza eneo lako la sasa na anwani ya unakoenda.

Ninatafsirije maandishi?

Kujifunza lugha mpya au kuelewa mabango katika nchi ngeni hakujawahi kuwa rahisi hivi. Na zana za utafsiri mtandaoni, unaweza ukatafsiri kwa haraka kila kitu kutoka vipande vidogo hadi wavuti kamili na sura za vitabu.
Google Translate ni moja ya zana za kutafsiri za bila malipo. Ili kutumia Google Translate vyema, tunapendekeza upitie kwa haraka mwongozo huu .

Ninatengenezaje alamisho?

Vivinjari vingi hukuruhusu uhifadhi mikato kwenye tovuti zako pendwa. Kwa kualamisha tovuti unazotembelea mara kwa mara, unaweza kuabiri haraka hadi kwa ukurasa bila kuchapa URL.
Unaweza pia kuhifadhi alamisho zako katika Akaunti yako ya Google. Unaweza kufikia alamisho hizi kutoka kompyuta yoyote yenye muunganisho wa Intaneti kutoka kwa Upau zana au Ukurasa wa kwanza wa Alamisho za Google.

Kuunganisha na kushiriki

Cloud computing ni nini?

Kwa kifupi, kila wakati unapotumia Intaneti, unatumia cloud computing. Maana ya hii ni kwamba, maelezo yote unayoyatafuta yamehifadhiwa kwenye seva katika maeneo mbalimbali duniani kote. Iwe unatazama video, unasoma habari au unasikiliza muziki, unapata maelezo kutoka kwa wingu, sio kutoka kwa diski kuu ya kompyuta yako.
Katika miaka ya karibuni, cloud computing imetoa hata faida zaidi. Sasa tunaweza kupakia faili zetu binafsi (picha, video, hati, muziki, nk.) kwa seva za wingu na kuzifikia kutoka kompyuta yoyote, hivyo kutulinda na kupoteza faili hizi kutokana na virusi, diski kuu zenye hitilafu, au makosa yetu wenyewe ya kibinadamu.

Programu za wavuti ni nini, na zinafanyaje kazi?

Ikiwa unacheza michezo mtandaoni, au unatumia kihariri picha mtandaoni, au unatumia huduma katika wavuti kama vile Google Maps, Twitter, Amazon, YouTube au Facebook, basi wewe ni mkaazi amilifu katika ulimwengu wa ajabu wa programu wavuti.
Programu za wavuti, pia zinazojulikana kama "programu" ni programu ambazo hukaa kwenye kivinjari chako au kwenye kifaa chako cha simu ya mkononi. Zinakuunganisha kwenye huduma za Intaneti ili kukuwezesha kufanya kazi rahisi, kama kualamisha tovuti na kuangalia barua pepe. Pia zinaweza kufanya kazi changamani kama vile kushiriki picha, kuabiri miji au kusikiliza muziki. Mfumo wako wa kawaida wa kuabiri gari ni mfano mzuri wa programu. Ndani ya programu hii, unaweza kupata maelezo katika muda halisi kulingana na eneo lako. Unaweza kupindua na kukuza ramani, pata maelekezo ya kuendesha gari, pata njia mbadala na tafuta maeneo maalum unayolenga kufikia.
Pamoja na ufikiaji, programu za wavuti ni salama zaidi. Kwa kuwa zinaendeshwa katika kivinjari chako, huhitaji kuzipakua kwenye kompyuta yako, hivyo kukulinda kutoka kwa virusi, programu hasidi na vidadisi. Sasa una ufikiaji mkubwa zaidi, na ufikiaji salama zaidi kuliko awali.
Kusoma zaidi juu ya programu za wavuti, chunguza kijitabu cha Vitu 20 Nilivyojifunza.

Programu huria ni nini?

Ili kuelewa "programu huria" ni nini, ni muhimu kwanza ufahamu "msimbo chanzo" ni nini. Msimbo chanzo ni lugha ambayo programu huandikwa kwayo. Ni lugha inayotumika katika vivinjari na programu ikielekeza programu jinsi ya kufanya kazi na kuishi.
“Programu huria” inamaanisha msimbo chanzo uko wazi na unapatikana kwa yeyote kuupitia. Unaweza kufanyia majaribio, geuza au ongeza, na tumia tena kwa ajili ya bidhaa au huduma zingine. Vivinjari vya mtandao vya Chrome na Firefox ni mfano wa programu za programu huria.

Barua pepe ni nini?

Barua pepe kwa kirefu ni barua ya elektroniki. Kutuma barua pepe ni sawa na kutuma toleo la elektroniki la barua. Unapotuma barua pepe yako, kwa kawaida inafika kwa mlengwa baada ya sekunde. Kama tu anwani ya nyumba, kila mtu ana anwani ya kipekee ya barua. Inakupasa ufungue akaunti ya barua pepe ili uweze kutuma na kupokea barua.
Ikiwa tayari unayo anwani ya barua pepe na unataka kufungua nyingine mpya, ni haraka na rahisi.

Ninapigaje gumzo mtandaoni?

Kupiga gumzo mtandaoni, kutumia video au kwa kutuma ujumbe, ni njia ya haraka ya kuungana na marafiki na familia walioko karibu na mbali. Huduma nyingi za mtandao hutoa vipengele vya kupiga gumzo mtandaoni, ikiwa ni pamoja na Google. Kwenye Google, unachotakiwa kufanya ili upige gumzo ni kuingia, alika marafiki zako, na uanzishe gumzo.

Ninapigaje simu kutoka kwenye kompyuta yangu?

Kuna huduma nyingi za mtandao zinazokuruhusu kutumia kompyuta ili kumpigia mtu simu. Nyingi ya huduma hizi zinakuhitaji usakinishe kipande cha programu au programu-jalizi, lakini unachohitaji tu ni muunganisho wa Intaneti, maikrofoni, na vipaza sauti na uko tayari kupiga simu.

Ninahamishaje faili kati ya kompyuta?

Ikiwa unayo faili kubwa au hata faili ndogo chache, unaweza kuzihamisha kutoka kompyuta hadi kompyuta kwa kutumia hifadhi pesi ya USB. Hifadhi pesi ya USB kimsingi ni kifaa kidogo cha hifadhi ambacho unaweza kuweka humo faili zako. Unapochomeka hicho kifaa kwenye kompyuta nyingine, unaweza buruta na uangushe faili hizo huko.

Mtandao jamii ni nini na ninadhibiti vipi ninachoruhusu watu wafahamu kunihusu?

Mtandao wa jamii ni tovuti au programu inayokuruhusu kuungana na marafiki na familia, na kushiriki taarifa, habari, picha na video. Mifano ya mitandao ya jamii tofauti ni pamoja na Facebook, Google+, Twitter and LinkedIn. Tovuti hizi ni baadhi ya kubwa kabisa kwenye Intaneti. Kuna zaidi ya watu bilioni moja kwenye Facebook, YouTube inatazamwa mara bilioni nne kila siku na Twitter ina zaidi ya watumiaji milioni 500. Mitandao ya jamii mingi inakuruhusu kurekebisha mipangilio yako – kukusadia kudhibiti maelezo yapi unayoshiriki, jinsi unavyoyashiriki, na unayashiriki na nani.

Google+ ni nini na ninaitumiaje?

Google+ husaidia kukuunganisha kwa unayejali na unachojali. Iliundwa na kushiriki halisi katika akili – na hiyo inamaanisha unaidhibiti. Google+ pia husaidia Google ikufanyie kazi bora – kufanya huduma unazozipenda tayari kuwa na kasi zaidi, yenye kuhusiana zaidi na ya kuaminika zaidi. Ili kuitumia vyema Google+, angalia maelezo zaidi juu ya vipengele vinavyopatikana kwako, ikiwa ni pamoja na Durara na Hangout.

YouTube, Blogger, na huduma nyingine za kuchapisha kwenye mtandao hufanyaje kazi?

Tovuti kama YouTube na Blogger huruhusu yeyote, popote kuungana na mabilioni ya watu duniani kote papo hapo. Kupitia mifumo mbalimbali mtandaoni – mitandao jamii, tovuti za video, zana za blogu, huduma za minada, na nyingine nyingi – watumiaji wa Intaneti wana uwezo wa kujenga maudhui, kuchapisha maelezo, kuwasiliana na kununua au kuuza bidhaa na huduma.

Ninapakiaje na kushiriki video kwenye YouTube?

Kuunda maudhui na kuyatangaza kwa ulimwengu kunakuwa sehemu muhimu ya kuwa raia anayeshiriki tarakinishi. Kupakia video yako kwenye YouTube ni rahisi. Ili kuanza, utahitaji kufungua akaunti ya Google. Ukishafungua akaunti, fuata hatua hizi rahisi ili kupakia video yako ya kwanza.

Ninadhibiti vipi sifa yangu ya tarakinishi?

Unapoanza kuunda na kupakia maudhui mtandaoni, chukua muda kidogo kufikiria kuhusu unachoshiriki na madhara yake kwa wengine. Unachokichapisha na maudhui unayopakia yatakuwakilisha mtandaoni. Hii pia inajulikana kama sifa ya tarakinishi. Usisahau hadhira isiyoonekana – wale wanaoweza kuona maudhui yako au kuyashiriki tena bila ufahamu wako. Kidokezo kinachofaa: ikiwa hutaki bibi yako ayaone, usiyachapishe.
Hakikisha unatembelea mipangilio yako ya faragha na usalama kwenye mifumo ya mitandao ya jamii kama vile Google+. Google hutoa zana kadhaa kwa ajili yako ili udhibiti mipangilio yako.

Post a Comment

 
Top