.post-body{ -webkit-touch-callout: none; -khtml-user-select: none; -moz-user-select: -moz-none; -ms-user-select: none; user-select: none; }

0

Kampuni ya Tesla Motors, inayounda betri ya gari, imetangaza kuwa, ina mpango wa kuuza teknolojia ya betri yenye uwezo wa kuzalisha kawi ya matumizi majumbani na kwenye biashara mbalimbali.
Bilionea muasisi wa Tesla, Elon Musk, anasema kuwa betri hiyo mpya itawezesha watu wengi kupata afueni kutokana na kuwa na uhakika wa nguvu za umeme bila ya kukatizwa.
Anasema kuwa teknolojia hiyo mpya itabadilisha mtizamo wa watu Duniani wa namna ya kutumia kawi.
Tesla
Tesla inapanga kwanza kuuza betri hizo nchini Marekani, mnamo miezi michache ijayo.
Tesla tayari inatengeneza betri zinazotumiwa na magari ya umeme yasotumia petrol.
Betri hizo, aina ya lithium-ion, huchajiwa mara-kwa-mara. Kwa teknolijia hiohio betri za kutumia majumbani na katika biashara zinatengenezwa.
Mmiliki wa Tesla Elon Musk
Mfumo huu wa betri unaitwa Powerwall wa vizio aina mbili: kizio cha 7kWh chauzwa $3,000 ilhali kizio cha 10kWh kwa $3,500.
Inakisiwa, Tesla itachuma $4.5bn kwa mauzo hayo. Lakini wadadisi wanadhani huenda Tesla ukakumbwa na ushindani mkubwa na makampuni mengine yenye masilahi hayo, kama General Elecctric na LG ya Korea Kusini.

Post a Comment

 
Top